
Msanii mkongwe wa muziki kutoka Morogoro, Afande Sele amedai
anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa madai anagawa pesa
kwa watu ili kuwashawishi wajitokeze katika maandamano ya UKUTA ambayo
yamepigwa marufuku.
Afande
Rapper huyo ambaye ni mwanasiasa na aligombea ubunge kupitia cha ACT
Wazalendo katika uchaguzi uliyopita, amedai yupo mikononi mwa polisi
toka jana.
“Huku ni kushindwa kama sio kufeli, toka jana nipo mikononi mwa polisi
eti naambiwa nimeratibu mkutano wa UKUTA , nimechapisha T-shirt na
kugawa fedha ili kesho watu waandamane, pia kuaandaa mkutano maeneo ya
Msamvu.,” aliandika Afande Sele kupitia facebook yake.
Aliongeza, “Nina zaidi ya mwezi sijakaa maeeneo ya Msamvu zaidi ya
kupita nikiwa naelekea mikoani tena nikiwa kwenye gari yangu. Ila hii
aibu na fedheha kwa jeshi la polisi, maamuzi ya kukurupuka . Tusubiri,”
COMMENT AND SHARE...................................................................
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!