Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa klabu ya YANGA
wanatarajia kuondoka jumamosi kwenda nchini GHANA kucheza mchezo wao
wa marudiano na MEDIAMA ya GHANA
Wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa klabu ya YANGA
wanatarajia kuondoka jumamosi kwenda nchini GHANA kucheza mchezo wao
wa marudiano na MEDIAMA ya GHANA katika michuano ya kombe la shirikisho.
YANGA wanaondoka wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya kufungana bao
moja kwa moja na MEDIAMA ya GHANA mchezo uliopigwa uwanja wa TAIFA
JIJINI DSM.
Katibu mkuu wa YANGA BARAKA DEUSDEDIT amesema timu inaondoka ikiwa na msafara wa watu 30 wachezaji 21 na viongozi tisa.
Baadhi ya wachezaji wa YANGA hawatasafiri na timu kutokana na kuwa
majeruhi na mwingine kuwa kadi mbili za njano, mchezaji VICENT BUSUU
anakadi mbili za njano , wakati GEOFREY MWASHUIYA atakuwa nje kwa muda
wa wiki tatu kutokana na kuumia goti wakati wa mchezo na SAGRADA
ESPERANCA ya ANGOLA na HAJI MWINYI itategemeana hali yake inavyoendelea
.
Kuhusu suala la mchezaji HASSAN RAMADHAN kuendelea kukalia
benchi baada ya kushindwa kufikia muafaka na klabu yake ya zamani ya
SIMBA uongozi wa kumuachia achezee YANGA , uongozi wa YANGA umesema
uliandika barua TFF kutatua tatizo hilo lakini hawakujibiwa.
YANGA haijafanya vizuri tangu kuingia hatua ya makundi ya michuano ya
kombe la shirikisho ambapo imepoteza michezo miwili katika michuano
hiyo ikifungwa na TP MAZEMBE nyumbani goli moja kwa bila na kufungwa na
MO BEJAIA ugenini goli moja kwa bila.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!