Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE DOKTA REHEMA NCHIMBI amewaagiza watumishi wa Serikali katika Mkoa huo Kuhakikisha wanawatumikia wananchi
Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE DOKTA REHEMA NCHIMBI amewagiza watumishi wa
Serikali katika Mkoa huo Kuhakikisha wanawatumikia wananchi na kutafuta
ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.
Dokta NCHIMBI amesema hayo kwenye kikao kazi kilichowakutanisha wakuu
wa Wilaya,wakurugenzi ,Wenyeviti wa Halmashauri,Viongozi Dini na
watumishi wa Ofisi yake.
Amewataka wakurugenzi kuhakikisha wanakua na takwimu sahihi za sekta
mbalimbali ili kufahamu kwa ufasaha jinsi ya kutekeleza majuku yao.
Suala la kupima maeneo na kuweka alama kwenye maeneo ya shule za
Msingi na Sekondari ili kuepuka Migogoro lilitiliwa mkazo pia katika
kikao hicho .
Kwa upande wao wenyeviti wa Halmashauri za MJI NJOMBE na MAKETE
wameelezea kubiliana na changamoto zinazowakabili katika upimaji maeneo
ya Shule.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!