Rapper Birdman ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa CASH MONEY records ambaye pia mchango wake upo kwenye muziki wa kina Nicki Minaj, Drake na Lil Wayne na wengine, amejikuta kwenye headlines leo baada ya kuamua kuondoka kwenye Interview ya Radio New York Marekani.
Birdman alikua mgeni kwenye show ya asubuhi THE BREAKFAST CLUB
na alipoingia tu studio kabla hajakaa alianza kwa kuwaonya Watangazaji
wa show hii kwamba wanatakiwa kuliheshimu jina lake na waache kumchezea.
Baada ya kukaa kwenye kiti Birdman
akiwa kaambatana na watu wake akiwemo mlinzi wake, alisema anachotaka ni
kwamba wanatakiwa kumuheshimu na waache kumchezea na kulichezea jina
lake zaidi ya hapo hataki kuongea kitu kingine chochote.
Pamoja na Birdman kuonyesha kuwa na
hasira, Watangazaji wa hii show walionekana ku-relax na walimtaka akae
aongee kwenye vipaza sauti na mbele ya camera kile alichotaka kuongea,
Birdman alisema angeweza kumfata mmoja wa Watangazaji hao mtaani tu
lakini ameamua kuja kuongea uso kwa uso kama Mwanaume.
Imeripotiwa Birdman amekasirishwa na
kitendo cha Watangazaji hawa kwenye baadhi ya show zao zilizopita
kumuongelea vibaya na anaona wanalichezea jina lake bila kujali na kumpa
heshima anayostahili kwa mchango wake kwenye muziki Marekani,
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!