Utafiti uliofanywa na Mtandao wa Mabadiliko
ya Tabia nchi umeonesha Tanzania imeshika nafasi ya nne katika ukanda wa
afrika mashariki
Utafiti uliofanywa na Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia nchi umeonesha
Tanzania imeshika nafasi ya nne katika ukanda wa afrika mashariki katika
matumizi ya fedha zinazotolewa katika kupambana na mabadiliko ya Tabia
nchi pamoja na kupunguza hewa ya ukaa.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa nchi ya Kwanza ni RWANDA ikifuatiwa na
KENYA, UGANDA na kisha baada ya Tanzania inafuata BURUNDI ambayo ni ya
mwisho kwakuwa SUDAN KUSINI haikuwa miongoni mwa nchi zilizofanyiwa
utafiti.
Kwamujibu wa Mratibu kutoka Mtandao wa Mabadiliko ya Tabia Nchi –CAN,
SIXBERT MWANGA miongoni mwa sababu zinazoelezwa kuwa nikisababishi cha
fedha hizo kutumika vibaya ni kutokuwepo kwa sera inayoeleza namna fedha
hizo zinavyoingia mpaka zinavyowanufaisha wananchi.
Wadau kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali wamesema
ili fedha hizi kutumika ipasavyo inapaswa serikali kutumia fedha hizo
kama zilizopangwa badala ya kuzipangia kazi nyingine.
Serikali pia imeshauriwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya
kiserikali katika kutengeneza na kusimamia miradi ili iweze kuwanufaisha
wananchi.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!