Waziri mkuu mpya wa UINGEREZA, THEREZA MAY, amesema licha ya kuwa uhusiano kati ya nchi ya UJERUMANI na nchi yake, utabadilika
Waziri mkuu mpya wa UINGEREZA, THEREZA MAY, amesema licha ya kuwa
uhusiano kati ya nchi ya UJERUMANI na nchi yake, utabadilika, baada ya
UINGEREZA kujitoa kwenye Umoja wan chi za ULAYA, lakini masuala ya
uchumi yatalazimika kuimarika.
Akizungumza mjini BERLIN, baada ya kukutana na mwenyeji wake Kansela
wa UJERUMANI, ANGELA MARKEL, akiwa katika ziara yake ya kwanza nje ya
nchi THEREZA, amesema uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili
unapaswa kuimarishwa zaidi.
Kwa upande wake ANGELA amesema, licha ya uamuzi wa wananchi wa
UINGEREZA, kujitoa kwenye umoja huo, wananchi wan chi hizo mbili bado
wana uhusiano wa karibu katika masuala mbalimbali. THEREZA anatarajiwa
kwenda UFARANSA, kukutana na rais FRANCOIS HOLLANDE wa nchi hiyo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!