Polisi
kanda maalum ya Dar es salaam leo July 22 2016 wametoa majumuisho ya
zoezi la uhakiki wa silaha mkoa wa Dar es salaam lililofanyika kwa miezi
mitatu, zoezi hilo lilianza March 1 2016 na limemalizika June 30 2016.
Kamishna
wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro ametoa taarifa
hiyo mbele ya wandishi wa habari na kusema idadi ya watu waliojitokeza
kuhakiki silaha kwa wilaya zote tatu ni 11,602 na jumla ya silaha 14107 zilihakikiwa.
Jumla ya
silaha 66 zilisalimishwa kutokana sababu mbalimbali ikiwamo mmiliki wa
silaha kuwa na umri mkubwa na kushindwa kumudu silaha. Zoezi la uhakiki
wa silaha limeiingizia Serikali mapato kiasi cha Mil 198.8
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!