Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno aliyeiongoza timu hiyo kutwaa Kombe la Euro 2016 katika historia Cristiano Ronaldo bado anaendelea na likizo yake na kuendelea kuuguza jeraha lake la goti, Ronaldo ambaye amewahi kuhusishwa kutaka kuihama Real Madrid ameweka wazi mpango wake na Real Madrid.
Ronaldo mkataba wake na
Real Madrid unamalizika 2018 na miaka miwili iliyopita alikuwa anahusishwa kutaka kuihama klabu hiyo na kutimkia katika vilabu vya
PSG,
Man United au kwenda kucheza Ligi ya Marekani MLS,
Ronaldo ameweka wazi walichozungumza kwenye simu na Rais wa
Real Madrid Florentino Perez.
Nimezungumza
na Rais kwenye simu lakini wakati nitakapo rudi Madrid tutaongea zaidi
kuhusiana na mkataba, kuongeza mkataba ni kitu ambacho nahitaji na
nimekuwa nikisema hili mara nyingi na klabu wanahitaji hivyo pia,
tuliongea kwa kifupi ila kila kitu kitakuwa sawa nikirudi”
Staa huyo wa kimataifa wa Ureno kwa sasa ana umri wa miaka 31 hadi atakapomaliza mkataba wake Real Madrid
2018, atakuwa na umri wa miaka 33 hivyo wengi walikuwa wanajua kuwa
msimu wa 2016/2017 huenda ukawa wa mwisho kwa staa huyo kuendelea
kusalia Santiago Bernabeu kwa maana atauzwa.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!