KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van Pluijm ameomba Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) kufanya mabadiliko kwa kuongeza idadi ya usajili wa
wachezaji wa kigeni kutoka 7 mpaka 10 kwenye timu zinazoshiriki Ligi
Kuu.
Pluijm alisema hayo kufuatia kufanya vibaya kwa timu hiyo kwenye
hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo
ilikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Medeama ya Ghana katikati ya
wiki hii.
Kwenye mahojiano maalumu na gazeti hili kwa njia ya mtandao jana
Pluijm alisema kwamba anahitaji kuijenga upya Yanga kwa ajili ya
mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao na aina ya wachezaji.
“Idadi ya wachezaji 10 wa kigeni ni muhimu kwa soka la Tanzania na
hasa kwa Yanga kwa sababu itashiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa
Afrika msimu ujao. Kama ikiwezekana idadi iongezwe nipate nafasi ya
kutengeneza upya kikosi cha ushindi,” alisema Pluijm.
“Tatizo langu ni pa kuwapata wachezaji wanaoweza kuimarisha Yanga. Hawapatikani katika ligi ya nyumbani.
Akizungumzia zaidi mchezo huo dhidi ya Madeama Pluijm aliwatupia
lawama mabeki wakongwe wa timu hiyo Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin
Yondani kwa kufanya makosa yaliyoigharimu timu hiyo kwenye mechi hiyo.
“Kila mmoja alisema ana furaha kuona Cannavaro akirejea kwenye kikosi
cha kwanza kwenye mechi hiyo. Lakini sasa kila mmoja aliona
alivyocheza. Nimehuzunishwa pia na kiwango cha Kelvin Yondani pia kwenye
mechi hii,” alisema Pluijm.
Suala la idadi ya wachezaji wa Ligi Kuu imekuwa ikibadilika mara kwa
mara, miaka ya nyuma klabu ziliruhusiwa kusajili wachezaji watatu,
baadaye ikaongezeka mpaka kufikia kusajili wachezaji watano lakini
watatu ndio wanaruhusiwa kucheza kwenye mechi moja.
Msimu uliopita TFF iliruhusu usajili wa wachezaji saba wa kigeni na
watano ndio wanaruhusiwa kucheza mechi moja. Baadhi ya klabu za Ligi Kuu
Azam, Yanga na Simba ziliomba kuruhusiwa kusajili wachezaji 10 wa Ligi
Kuu jambo ambalo halijapatiwa jibu na TFF.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!