Mwanamuziki wa Nigeria anayeunda kundi la Psquare Peter Okoye ameomba msamaha kwa washabiki kufuatia ugomvi na kaka yake
Kupitia video iliyosambaa katika mitandao ya kijamii amesema timu nzima ya Psquare kwa sasa imerudi tena pamoja.
Akiwa amevalia kofia ndani ya gari, video hiyo inamuonesha Okoye ni
mwenye kujuta, akisema kuwa anabeba jukumu kwa yote yaliyotokea.
Peter alikuwa na uhasama na pacha wake Paul, ambaye ndiye amekuwa
akiimba naye kwa zaidi ya muongo mmoja, hali iliyofanya kugawa kundi
hilo.
Kulikuwa na dalili kwamba utengano wao huo unahatarisha mafanikio ya mapacha hao.
Peter na Paul wametoa nyimbo nyingi zilizovuma ndani ya Nigeria na nchi nyingine za Afrika.
Hivi karibuni mwanamuziki wa Tanzania DIAMOND PLATNUMS ametoa wimbo
wa KIDOGO aliowashirikisha ndugu hao wawili wa kundi la PSQUARE
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!