Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu –NIMR- DKT. MWELE MALECELA amesema endapo tafiti za tiba zinazofanywa
Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya binadamu –NIMR- DKT.
MWELE MALECELA amesema endapo tafiti za tiba zinazofanywa zitalenga
katika ugunduzi wa magonjwa sugu yanayoisumbua jamii zitakuwa na
manufaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini DAR ES SALAAM amesema
matokeo ya tafiti hizo yanaweza kugundua tiba sahihi ya magonjwa
yanayoisumbua jamii.
Aidha amesema Mkurugenzi wa taasisi ya Afya ya MAREKANI DKT, FRANSIS
COLLINS anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini kuanzia Julai 31
mwaka huu kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali inayofadhiliwa na nchi
hiyo.
Kwa upande wao MKURUGENZI wa Makamu Mkuu wa chuo kikuu kishiriki cha
Afya Profesa EPHATA KAAYA na Mtafiti kiongozi wa afya wa Tume ya sayansi
na teknolojia DKT. KHADIJA MALIMA wamesema ushirikiano wa kitafiti kati
ya TANZANIA na MAREKANI umekuwa na manufaa.
Hata hivyo wamesema kuna haja kwa sasa kubadili mbinu za tafiti kwa lengo la kuboresha mazingira ya utendaji wake
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!