MANCHESTER CITY, wakicheza mechi yao ya kwanza ya kujiandaa kwa msimu
mpya chini ya meneja mpya PEP GUARDIOLA, wamechapwa bao moja kwa bila na
klabu ya zamani ya meneja huyo BAYERN MUNICH CITY walifungwa bao moja na ERDAL OZTURK wa BAYERN, ambao kwa sasa mkufunzi wao ni CARLO ANCELOTTI.
Wachezaji wengi nyota hawakucheza mechi hiyo kwani bado wanapumzika baada ya kushiriki Euro 2016 na Copa America.
GUARDIOLA alichezesha wachezaji 12 wa timu ya vijana, mechi hiyo iliyochezewa ALLIANZ ARENA.
Mlinda lango wao alikuwa ANGUS GUNN, mwanawe mchezaji nyota wa zamani wa NORWICH BRYAN.
CITY sasa wataelekea Uchina ambapo watacheza dhidi ya MANCHESTER UNITED siku ya Jumatatu.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!