Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema katika kila saa moja watu wanaokadiriwa 400 wanakufa barani AFRIKA.
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amesema katika kila saa moja watu
wanaokadiriwa 400 wanakufa barani AFRIKA kutokana na magonjwa
yanayosabishwa na maji.
Makamu wa Rais amesema hayo Jijini DSM alipokua akifungua mkutano
uliojumuisha nchi 30 wenye lengo la kujadili changamoto za maji barani
AFRIKA kwa ajili ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu katika
usalama wa maji safi na salama.
SAMIA SULUHU HASSAN amesema Idadi kubwa ya watu barani Afrika wanakabiliwa na uhaba wa huduma ya maji safi na salama.
Mkutano wa maji barani Afrika unatazamwa kama sehemu muhimu ya
kuboresha utoaji wa huduma ya maji nchini,ambayo dira ya taifa ya
maendeleo ya mwaka 2025 inadhamiria kumaliza tatizo la maji nchini.
Baadhi ya washiriki katika mkutano huo wamesema baadhi
ya miradi imekosa usimamizi na wameshauri serikali za Afrika kutoa
elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu utunzaji wa miradi ya maji .
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!