Katibu
mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amekuwa na
ziara nje ya nchi tangu baada ya uchaguzi mkuu wa marudio Zanzibar March
2016 kuisha, Maalim Seif amekuwa akienda jumuiya za kimataifa kwa ajili
ya kutafuta kile anachokiita haki kutokana na uchaguzi mkuu wa Zanzibar
October 2015 kufutwa.
Leo
July 21 2016 Naibu katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Nassor Mazrui
amekutana na waandishi wa habari ambapo aliulizwa mchakato wa kufungua
kesi katika mahakama ya kimataifa ya ICC ili kudai haki yao kama
walivyosema hapo awali.
Mazrui
amesema kuwa leo au kesho Maalim Seif anatarajiwa kufika katika
mahakama ya kimataifa ya ICC, The Hague nchini Uholanzi katika harakati
zake za kudai haki katika uchaguzi uliofanyika october 2015…….
>>>’naamini
kama si leo au kesho Maalim Seif atakuwa the Hague kwenda kuelezea
namna gani demokrasia ya Zanzibar na Tanzania inavyominywa kwa hivyo
suala la ICC tumelipania na lazima hiyo kesi itakwenda na kila
aliyedhulumiwa, aliyedhulumu atafika katika mahakama ya ICC‘ >>>>> Usisahau kulike, share na kukoment
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!