Habari kutoka nchini KENYA zinasema, majeshi ya serikali ya nchi hiyo
yamempiga risasi na kumuua mtu mmoja anayesemekana ni mpiganaji wa
kikundi cha AL SHABAAB
Habari kutoka nchini KENYA zinasema, majeshi ya serikali ya nchi hiyo
yamempiga risasi na kumuua mtu mmoja anayesemekana ni mpiganaji wa
kikundi cha AL SHABAAB cha nchini SOMALIA, aliyekuwa akishikiliwa nchini
humo.
Mtu huyo aliyekuwa akishikiliwa katika kituo cha Polisi cha PENGURIA,
alimpora polisi moja bunduki na kuanza kuwafyatulia risasi askari
waliokuwa katika eneo hilo.
Habari zinasema askari wanne waliuawa katika tukio hilo.
Serikali ya KENYA imesema askari wanadhibiti eneo hilo la kituo cha
polisi baada ya kulizingira kwa saa kadhaa ikiwa ni katika jitihada za
kumdhibiti mtu huyo.
Mpiganajo huyo wa kikundi cha AL SHABAAB alikuwa akijaribu kuwaokao wapiganaji wengine waliokuwa wakishikiliwa kituoni hapo.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!