Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM Taifa anayemaliza muda wake
Dakta JAKAYA KIKWETE amewataka wanachama wa chama hicho kuwa kitu kimoja
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM Taifa anayemaliza muda wake
Dakta JAKAYA KIKWETE amewataka wanachama wa chama hicho kuwa kitu kimoja
ili kuepusha chama hicho kuyumbishwa na watu wasioitakia mema CCM.
Pamoja na kusisitiza suala la umoja, Dakta KIKWETE amewashukuru
viongozi wa CCM waliotangulia na kumtaka Mwenyekiti mpya wa chama hicho
Rais dakta JOHN MAGUFULI kuwa kiongozi bora wakati wote wa uongozi wake.
Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu,aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM
Dkt. JAKAYA KIKWETE amesema ana imani kubwa na Rais Dakta. MAGUFULI kwa
kazi nzuri anayoifanya kwa kutekeleza Ilani ya CCM na kumsihi kuunda
timu imara itakayomsaidia kutekeleza majukumu yake.
Mwenyekiti mpya wa CCM Dkt. JOHN MAGUFULI anakuwa mwenyekiti wa TANO
akitanguliwa na Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE,
Mzee ALI HASSAN MWINYI , Mzee BENJAMIN MKAPA na Dkt. JAKAYA KIKWETE.
Share And Comment Bellow On What You Think About This Post!!!
Comments
Post a Comment
Welcome.......
What are you thinking of....!!